Friday, February 15, 2013

PANDA SHUKA YA UHUSIANO BAINA YA AFRIKA NA CHINA!!



China na Bara la Afrika zimekuwa na uhusiano wa tangu na tangu kwenye biashara kutokana na itikadfi ambayo imeikuwa ikitumiwa na serikali ya Muasisi wa Taifa hilo Mao Zedong.

China inaongozwa na itikadi za Kijamaa ambazo zimekuwa zikitumiwa kwa miaka mingi na Mataifa ya kutoka Bara la Afrika kitu ambacho kimechagiza uhusiano baina ya pande hizi mbili kushika kasi zaidi.

Uhusiano huu ulianza katika karne ya kumi na nne ambapo chini ilionesha utayari wake wa kuja Afrika na kuhakikisha wanafanya biashara na mataifa yanayopatikana kwenye eneo hili kitu ambacho walifanikiwa mno.

China ilianzisha biashara katika eneo la Pwani ya Bahari ya Hindi kuanzia kwenye Pembe ya Afrika kunako nchi ya Somalia hadi kufika eneo la Kusini kwenye nchi ya Msumbiji.

Uwekezaji wa China Barani Afrika ulipamba moto ilipofika miaka ya 1980 kwani waliweza kuwekeza jumla ya dola bilioni moja kwenye sekta mbalimbali kitu ambacho kionekana si kitisho kwa wakati huo.

China ilizidisha uwekezaji wake kwa kasi mno Barani Afrika kwani kufika kipindi cha miaka ya 1990 walizidisha uwekezsaji wao kwa asilimia 700 kitu kilichoyashtua Mataifa ya Magharibi yakiwemo Marekani na Uingereza.

China ikaendelea kujidhatiti zaidi Barani Afrika kwani ilipofika mwaka 2000 ikaanzisha uhusiano kupitia Jukwaa la Ushirikiano Baina ya China-Afrika FOCAC hatyua iliyowafanya wajikite zaidi kwenye kuwekeza.

Kwa sasa China ndiyo nchi inayoonekana kuwekeza zaidi Barani Afrika kwani ina jumla ya Makampuni 800 yanayoendesha shughuli zake huku kipindi cvha miezi 10 ya mwaka 2012 ukionesha wamewekeza dola bilioni 163.9.

Makampuni kutoka China yaliyokuja kuwekeza Barani Afrika yamehifadhi pesa zaidi kwenye:
·        Sekta ya Nishati
·        Miundombinu
·        Sekta ya Kilimo
·        Sekya ya Afya
·        Sekta ya Fedha (Benki)
·        Elimu

Sekta ya Nishati: China imekuwa ikitegemea theluthi moja ya mafuta inayotumia kwenye nchi hiyo kutoka Barani Afrika. Mafuta hayo yamekuwa yakichimbwa kutoka nchi za Ngieria, Sudan na Angola. Makampuni ya China yamefanya uwekezaji mkubwa katika nchi hizo mbili. China imeweza kuwekeza kwenye mafuta na gesi huku wakiwa wametumia jumla ya dola bilioni 2 hadi sasa.

Miundombinu: Uwekezaji wa serikali ya China kwenye mkundombinu umekuwa ukifanyika wakati mwingine kama msaada au mkopo. Mara nyingi uwekezaji wao umekuwa ukilenga sehemu ambazo wamekuwa wakifanya biashara za mafuta na gesi. China imekuwa ikijenga barabara na hata reli katika kuhakikisha bidhaa ambazo wanazizalisha Barani Afrika ziweze kusafirishwa kwa urahisi. China pia ilikuwa nchi ya kwanza kujenga reli nyingi Barani Afrika na hata nchini Tanzani.

Sekta ya Kilimo: China imekuwa mwekezaji mzuri kwenye sekta ya kilimo Barani Afrika ambapo kwa sasa wametumia dola bilioni 80.5 katika kipindi cha miezi mitano pekee ya mwaka 2012. Uwekezaji mkubwa wamekuwa wakiufanya katika nchi za Benin, Burkina Faso pamoja na Mali. Uwekezaji na biashara ya kilimo imekuwa ikiongezeka kila mwaka hasa kwenye mataifa ambayo China imewekeza zaidi.

Mtaalam kutoka nchini China akitoa maelezo kwa wakulima wa Mpunga Barani Afrika
Sekta ya Afya: Serikali ya China imekuwa ikitumia diplomasia ya afya katika nchi za Bara la Afrika kwa kutoa msaada tangu miaka ya 1960. Takwimu zinaonesha katika kipindi cha 1960 hadi 2005 zaidi ya Madaktari 15,000 kutoka China walikuja kutoa matibabu Barani Afrika na kuwafikia watu milioni 170 katika nchi 47. China pia imejenga hospital 31 na vituo vya afya 145 nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC kama sehemu ya kusaidia masuala ya afya.

Sekta ya Fedha (Benki): Licha ya China kufanyabiashara ya Mataifa ya Afrika lakini imekuwa ikiwekeza kwa kiwango cha hali ya juu katika sekta ya benki. Wawekezaji kutoka China wamekuwa wakifungua mabenki huku wananchi wao wakiwa wateja wakubwa wa mabenki hayo.
  
Elimu: Elimu ni moja ya sehemu ambayo China imefanya uwekezaji mkubwa sana ambapo wanafunzi wengi kutoka Afrika wamekuwa wakipata ufadhili wa masomo. Vijana wengi wamekuwa wakienda China kusoma japokuwa Taifa hilo limekuwa likitumia fursa hiyi kusambaza utamaduni wao ikiwemo kufuza Kichina.

Makampuni kutoka China yamezidi kujizolea umaarufu mkubwa ndani ya Bara la Afrika na hivyo hata biashara yao kukuwa zaidi tofauti na ilivyokuwa awali ambapo  Marekani ilikuwa kinara wa wawekezaji.

Uwekezaji wa China katika Bara la Afrika umekuwa na tija kwa mataifa ambayo yameweza kunufainika kwenye masuala yafuatayo:
·        Miundombinu
·        Utalii
·        Elimu
·        Afya
·        Biashara
·        Ajira
·        Michezo

Miundombinu: Nchi za Bara la Afrika zimekuwa zikinufaika na uwekezaji wa China hasa kwenye suala la miundombinu. Serikali ya China imekuwa ikilazimika kujenga barabara na reli kwa msaada lakini hata kwa mkopo. China inafanya hivyo kwa sasa imekuwa ikihitaji kupata urahisi wa kufika maeneo mbalimbali yenye rasilimali Barani Afrika.

Utalii: Bara la Afrika limebarikiwa kuwa na hazina kubwa ya sehemu za vivutio vya utalii ambavyo vimekuwa vikitembelewa na raia wa kigeni. Wananchi kutoka China ni miongoni mwa wageni ambao wanakuja kuangalia vivutio hivyo na kuchangia katika pato la mataifa ya Afrika.

Elimu: Vijana kutoka Afrika wamekuwa wakipata elimu kutoka nchini China bila ya wao kulazimika kulipia fedha. Hii ni moja ya sehemu ambayo serikali za Afrika zinaokoa fedha za kuwasomesha wananchi wake wanaopatiwa ufadhili kutoka China. Kwenye elimu pia kuna mpango wa kubadilishana wanafunzi unaowasaidia wanafunzi kutoka Barani Afrika.

Afya: Bara la Afrika limekuwa likipata nafuu kubwa mno kutoka China kwenye sekta ya afya. Serikali ya China imekuwa mstari wa mbele kujenga Hospital na Zahanati katika Bara la Afrika pamoja na kutoa madaktari wake Bingwa. Magonjwa kama malaria na kifua kikuu yamekuwa yakipatiwa kipaumbele kimatibabu kutoka China.

Biashara: Biashara ambayo imekuwa ikifanyika baina ya Afrika na China imekuwa ikitoa nafasi kwa bidhaa kutoka Bara hili kuuzwa katika soko la China. Hiki ni kitu kikubwa ambacho kimesaidia baadhi ya nchi kupata soko la bidhaa zao ughaibuni. Afrika pia imekuwa ikinufaika na bidhaa za bei nafuu zinazotengenezwa kutoka China. Viwanda vya China vimekuwa vikiuza bidhaa kulingana na kipatyo cha mnunuzi.

Ajira: Serikali ya China imekuwa ikitoa ajira kwa wananchi wengi wa Mataifa ya Afrika. Kutolewa kwa ajira hizo kumerahisisha mkakati wa serikali husika kukabiliana na tatizo la ajira linaloonekana kuwa sugu. Jumla ya Waafrika 20,000 wanafanyakazi nchini China na hizi zikiwa ajira rasmi.

Michezo: Sekta ya michezo Barani Afrika imekuwa ikinufaika na uhusianio uliopo baina ya Bara hili na nchi ya China. Serikali ya China imeweza kujenga viwanja vingi vya kisasa Barani Afrika kwa kushirikiana na serikali husika. Msumbiji, Tanzania, Uganda na hata Sudan ni miongoni mwa waliofaidika kwa kupata viwanuja hivyo vya kisasa. Viwanja hivyo vimekuwa chachu ya maendeleo ya michezo katika nchi husika.

Ujenzi wa Uwanja wa Mpira wa Miguu ukiendelea chini ya uongozi wa Wakandarasi kutoka China
China imeendelea kukabiliwa na upinzani kutoka kwa washindani wake wa kibiashara wakiwemo Marekani na Uingereza ambao wanakosoa mno siasa za taifa hilo na itikadi zao, uchumi wao na namna wanavyojikita barani Afrika pamoja na msaada wa kijeshi wanaoutoa kwa nchi husika.

Mitazamo hiyo imekuwa haiishii kwa mataiga hayo tu mawili lakini pia wananchi wa Afrika wamekuwa wakiutazama uhusiano baina ya Bara lao na China kwa mitazamo tofauti ikiwemo ifuatayo:
·        Kuua Soko
·        Kuua Viwanda
·        Kushuka kwa Bei

Kuua Soko: Wafanyabiasha wengi wamekiwa wakilalamika uhusiano baina ya China na Afrika umechangia pakubwa kuua soko la ndani la kutokana na bidhaa nyingi kuingizwa kutoka nje. Wafanyabiashara hao wanaoana soko kubwa ambalo walikuwa wanalitegemea limechukuliwa na bidhaa kutoka China ambayo mara nyingi imekuwa ikiuza bidhaa zake kwa bei rahisi.

Kuua Viwanda: China imekuwa ikinyooshewa kidole cha lawama kama moja ya sababu kubwa ya kufa kwa viwanda vya Afrika. Viwanda vimekuwa vinakufa kutokana na kufanya uzalishaji ambao unakusa soko la bidhaa wanazolizalisha kutokana na kuelemewa na bidhaa za kutoka nuje hasa China.

Kushuka kwa Bei: Wananchi wengi kutoka Afrika kwa kipindi kirefu wamekuwa wanunuzi wakubwa wa bidhaa kutoka China na hii kwa sababu bei yake imekuwa ya chini ukilinganisha na nyingine. Wananchi wamekuwa wakifurahishwa na uingizwaji wa bidhaa hizo za bei rahisi kwa madai wanazimudu kulingana na wakati wao bila ya kujali umadhubuti wake.

Uhusiano baina ya China na Bara la Afrika umekuwa na faida na hasara zake hasa kwa mataifa ya Afrika lakini umeendelea kutokana na uwepo wa uhusiano mzuri wa kidiplomasia baina ya pande hizo mbili.

Swali la kujiuliza kwa sasa ni je Afrika imekuwa ikipata manufaa ya kutosha kutoka kwa China ukilinganisha nay ale ambayo walikuwa wanayapata kutoka kwa Mataifa ya Magharibi ikiwemo Marekani na Uingereza???

No comments:

Post a Comment