China na Bara la
Afrika zimekuwa na uhusiano wa tangu na tangu kwenye biashara kutokana na itikadfi
ambayo imeikuwa ikitumiwa na serikali ya Muasisi wa Taifa hilo Mao
Zedong.
China inaongozwa
na itikadi za Kijamaa ambazo zimekuwa zikitumiwa kwa miaka mingi na Mataifa ya
kutoka Bara la Afrika kitu ambacho kimechagiza uhusiano baina ya pande hizi
mbili kushika kasi zaidi.
Uhusiano huu
ulianza katika karne ya kumi na nne ambapo chini ilionesha utayari wake wa kuja
Afrika na kuhakikisha wanafanya biashara na mataifa yanayopatikana kwenye eneo
hili kitu ambacho walifanikiwa mno.
China ilianzisha
biashara katika eneo la Pwani ya Bahari ya Hindi kuanzia kwenye Pembe ya Afrika
kunako nchi ya Somalia hadi kufika eneo la Kusini kwenye nchi ya Msumbiji.
Uwekezaji wa
China Barani Afrika ulipamba moto ilipofika miaka ya 1980 kwani waliweza
kuwekeza jumla ya dola bilioni moja kwenye sekta mbalimbali kitu ambacho
kionekana si kitisho kwa wakati huo.
China ilizidisha
uwekezaji wake kwa kasi mno Barani Afrika kwani kufika kipindi cha miaka ya
1990 walizidisha uwekezsaji wao kwa asilimia 700 kitu kilichoyashtua Mataifa ya
Magharibi yakiwemo Marekani na Uingereza.
China ikaendelea
kujidhatiti zaidi Barani Afrika kwani ilipofika mwaka 2000 ikaanzisha uhusiano
kupitia Jukwaa la Ushirikiano Baina ya China-Afrika FOCAC hatyua iliyowafanya
wajikite zaidi kwenye kuwekeza.
Kwa sasa China
ndiyo nchi inayoonekana kuwekeza zaidi Barani Afrika kwani ina jumla ya
Makampuni 800 yanayoendesha shughuli zake huku kipindi cvha miezi 10 ya mwaka
2012 ukionesha wamewekeza dola bilioni 163.9.
Makampuni kutoka
China yaliyokuja kuwekeza Barani Afrika yamehifadhi pesa zaidi kwenye:
·
Sekta
ya Nishati
·
Miundombinu
·
Sekta
ya Kilimo
·
Sekya
ya Afya
·
Sekta
ya Fedha (Benki)
·
Elimu
Sekta ya Nishati: China imekuwa ikitegemea theluthi moja ya mafuta
inayotumia kwenye nchi hiyo kutoka Barani Afrika. Mafuta hayo yamekuwa
yakichimbwa kutoka nchi za Ngieria, Sudan na Angola. Makampuni ya China yamefanya
uwekezaji mkubwa katika nchi hizo mbili. China imeweza kuwekeza kwenye mafuta
na gesi huku wakiwa wametumia jumla ya dola bilioni 2 hadi sasa.
Miundombinu: Uwekezaji wa serikali ya China kwenye mkundombinu
umekuwa ukifanyika wakati mwingine kama msaada au mkopo. Mara nyingi uwekezaji
wao umekuwa ukilenga sehemu ambazo wamekuwa wakifanya biashara za mafuta na
gesi. China imekuwa ikijenga barabara na hata reli katika kuhakikisha bidhaa
ambazo wanazizalisha Barani Afrika ziweze kusafirishwa kwa urahisi. China pia
ilikuwa nchi ya kwanza kujenga reli nyingi Barani Afrika na hata nchini
Tanzani.
Sekta ya Kilimo: China imekuwa mwekezaji mzuri kwenye sekta ya kilimo
Barani Afrika ambapo kwa sasa wametumia dola bilioni 80.5 katika kipindi cha
miezi mitano pekee ya mwaka 2012. Uwekezaji mkubwa wamekuwa wakiufanya katika
nchi za Benin, Burkina Faso pamoja na Mali. Uwekezaji na biashara ya kilimo
imekuwa ikiongezeka kila mwaka hasa kwenye mataifa ambayo China imewekeza
zaidi.
|
Mtaalam kutoka nchini China akitoa maelezo kwa wakulima wa Mpunga Barani Afrika |
Sekta ya Afya: Serikali ya China imekuwa ikitumia diplomasia ya afya
katika nchi za Bara la Afrika kwa kutoa msaada tangu miaka ya 1960. Takwimu
zinaonesha katika kipindi cha 1960 hadi 2005 zaidi ya Madaktari 15,000 kutoka
China walikuja kutoa matibabu Barani Afrika na kuwafikia watu milioni 170
katika nchi 47. China pia imejenga hospital 31 na vituo vya afya 145 nchini
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC kama sehemu ya kusaidia masuala ya afya.
Sekta ya Fedha (Benki): Licha ya China kufanyabiashara ya Mataifa ya Afrika
lakini imekuwa ikiwekeza kwa kiwango cha hali ya juu katika sekta ya benki.
Wawekezaji kutoka China wamekuwa wakifungua mabenki huku wananchi wao wakiwa
wateja wakubwa wa mabenki hayo.
Elimu: Elimu ni moja ya sehemu ambayo China imefanya uwekezaji mkubwa sana ambapo
wanafunzi wengi kutoka Afrika wamekuwa wakipata ufadhili wa masomo. Vijana
wengi wamekuwa wakienda China kusoma japokuwa Taifa hilo limekuwa likitumia
fursa hiyi kusambaza utamaduni wao ikiwemo kufuza Kichina.
Makampuni kutoka
China yamezidi kujizolea umaarufu mkubwa ndani ya Bara la Afrika na hivyo hata
biashara yao kukuwa zaidi tofauti na ilivyokuwa awali ambapo Marekani ilikuwa kinara wa wawekezaji.
Uwekezaji wa
China katika Bara la Afrika umekuwa na tija kwa mataifa ambayo yameweza
kunufainika kwenye masuala yafuatayo:
·
Miundombinu
·
Utalii
·
Elimu
·
Afya
·
Biashara
·
Ajira
·
Michezo
Miundombinu: Nchi za Bara la Afrika zimekuwa zikinufaika na
uwekezaji wa China hasa kwenye suala la miundombinu. Serikali ya China imekuwa
ikilazimika kujenga barabara na reli kwa msaada lakini hata kwa mkopo. China
inafanya hivyo kwa sasa imekuwa ikihitaji kupata urahisi wa kufika maeneo
mbalimbali yenye rasilimali Barani Afrika.
Utalii: Bara la Afrika limebarikiwa kuwa na hazina kubwa ya sehemu za vivutio
vya utalii ambavyo vimekuwa vikitembelewa na raia wa kigeni. Wananchi kutoka
China ni miongoni mwa wageni ambao wanakuja kuangalia vivutio hivyo na
kuchangia katika pato la mataifa ya Afrika.
Elimu: Vijana kutoka Afrika wamekuwa wakipata elimu kutoka nchini China bila
ya wao kulazimika kulipia fedha. Hii ni moja ya sehemu ambayo serikali za
Afrika zinaokoa fedha za kuwasomesha wananchi wake wanaopatiwa ufadhili kutoka
China. Kwenye elimu pia kuna mpango wa kubadilishana wanafunzi unaowasaidia
wanafunzi kutoka Barani Afrika.
Afya: Bara la Afrika limekuwa likipata nafuu kubwa mno kutoka China kwenye
sekta ya afya. Serikali ya China imekuwa mstari wa mbele kujenga Hospital na
Zahanati katika Bara la Afrika pamoja na kutoa madaktari wake Bingwa. Magonjwa
kama malaria na kifua kikuu yamekuwa yakipatiwa kipaumbele kimatibabu kutoka
China.
Biashara: Biashara ambayo imekuwa ikifanyika baina ya Afrika na China imekuwa
ikitoa nafasi kwa bidhaa kutoka Bara hili kuuzwa katika soko la China. Hiki ni
kitu kikubwa ambacho kimesaidia baadhi ya nchi kupata soko la bidhaa zao
ughaibuni. Afrika pia imekuwa ikinufaika na bidhaa za bei nafuu
zinazotengenezwa kutoka China. Viwanda vya China vimekuwa vikiuza bidhaa
kulingana na kipatyo cha mnunuzi.
Ajira: Serikali ya China imekuwa ikitoa ajira kwa wananchi wengi wa Mataifa ya
Afrika. Kutolewa kwa ajira hizo kumerahisisha mkakati wa serikali husika
kukabiliana na tatizo la ajira linaloonekana kuwa sugu. Jumla ya Waafrika
20,000 wanafanyakazi nchini China na hizi zikiwa ajira rasmi.
Michezo: Sekta ya michezo Barani Afrika imekuwa ikinufaika na uhusianio uliopo
baina ya Bara hili na nchi ya China. Serikali ya China imeweza kujenga viwanja
vingi vya kisasa Barani Afrika kwa kushirikiana na serikali husika. Msumbiji,
Tanzania, Uganda na hata Sudan ni miongoni mwa waliofaidika kwa kupata viwanuja
hivyo vya kisasa. Viwanja hivyo vimekuwa chachu ya maendeleo ya michezo katika
nchi husika.
|
Ujenzi wa Uwanja wa Mpira wa Miguu ukiendelea chini ya uongozi wa Wakandarasi kutoka China |
China imeendelea
kukabiliwa na upinzani kutoka kwa washindani wake wa kibiashara wakiwemo
Marekani na Uingereza ambao wanakosoa mno siasa za taifa hilo na itikadi zao,
uchumi wao na namna wanavyojikita barani Afrika pamoja na msaada wa kijeshi
wanaoutoa kwa nchi husika.
Mitazamo hiyo
imekuwa haiishii kwa mataiga hayo tu mawili lakini pia wananchi wa Afrika
wamekuwa wakiutazama uhusiano baina ya Bara lao na China kwa mitazamo tofauti
ikiwemo ifuatayo:
·
Kuua
Soko
·
Kuua
Viwanda
·
Kushuka
kwa Bei
Kuua Soko: Wafanyabiasha wengi wamekiwa wakilalamika uhusiano
baina ya China na Afrika umechangia pakubwa kuua soko la ndani la kutokana na
bidhaa nyingi kuingizwa kutoka nje. Wafanyabiashara hao wanaoana soko kubwa
ambalo walikuwa wanalitegemea limechukuliwa na bidhaa kutoka China ambayo mara
nyingi imekuwa ikiuza bidhaa zake kwa bei rahisi.
Kuua Viwanda: China imekuwa ikinyooshewa kidole cha lawama kama
moja ya sababu kubwa ya kufa kwa viwanda vya Afrika. Viwanda vimekuwa vinakufa
kutokana na kufanya uzalishaji ambao unakusa soko la bidhaa wanazolizalisha
kutokana na kuelemewa na bidhaa za kutoka nuje hasa China.
Kushuka kwa Bei: Wananchi wengi kutoka Afrika kwa kipindi kirefu
wamekuwa wanunuzi wakubwa wa bidhaa kutoka China na hii kwa sababu bei yake
imekuwa ya chini ukilinganisha na nyingine. Wananchi wamekuwa wakifurahishwa na
uingizwaji wa bidhaa hizo za bei rahisi kwa madai wanazimudu kulingana na
wakati wao bila ya kujali umadhubuti wake.
Uhusiano baina
ya China na Bara la Afrika umekuwa na faida na hasara zake hasa kwa mataifa ya
Afrika lakini umeendelea kutokana na uwepo wa uhusiano mzuri wa kidiplomasia
baina ya pande hizo mbili.
Swali la
kujiuliza kwa sasa ni je Afrika imekuwa ikipata manufaa ya kutosha kutoka kwa
China ukilinganisha nay ale ambayo walikuwa wanayapata kutoka kwa Mataifa ya
Magharibi ikiwemo Marekani na Uingereza???